Mkazi wa Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, Oscar Edgar Embedodo, ametahadharisha wananchi wa Sumbawanga na Watanzania kwa ujumla juu ya hatari ya kushawishiwa kususia uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Amesema kuwa ushawishi huo si wa kawaida, bali ni kiashiria cha mpango wa kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi binafsi ya kisiasa.
Embedodo ameonya kuwa baadhi ya watu wenye nia ovu tayari wameanza kuhamisha familia zao na kuzipeleka katika nchi zinazowafadhili kuleta vurugu ndani ya Tanzania. Amehoji kuwa kama kweli watu hao wanamaanisha amani na ustawi wa taifa, kwa nini familia zao hazipo nchini kushuhudia matokeo ya kile wanachohubiri?
Ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini, kuwahoji na kutowafuata viongozi wa namna hiyo. Amewahimiza wajitayarishe kushiriki kikamilifu katika uchaguzi kwa amani, kwa kuwa uchaguzi ni haki ya msingi ya kila raia na njia ya kujenga taifa lenye maendeleo na mshikamano wa kweli.
#MSLAC #Katibanasheria #Hakingowi #SisiTanzania #Katibanasheria
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+