KAMPENI YA “NO REFORMS NO ELECTION” INAMPANGO WA KUIPENDELEA TEAM – ELISHA ASA MWAMBENE

Elisha Asa Mwambene, Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mtaa wa Msasani, Tunduma, Mkoa wa Songwe, ameibua mjadala mzito kuhusu kampeni ya “No Reforms No Election” inayoendeshwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Tundu Lissu.

Kupitia mahojiano na wanahabari, Elisha amesema vijana wengi Tunduma wameshindwa kuelewa lengo hasa la kampeni hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho tayari wameshatangaza nia ya kugombea nafasi za ubunge katika uchaguzi ujao.

Kwa mujibu wa Elisha, kampeni ya Lissu inaonekana kuwa na ajenda ya siri ya kuingiza “Team Lissu” bungeni huku ikilenga kuiweka pembeni “Team Mbowe”, jambo ambalo linaweza kuligawa na kulidhoofisha chama.

Ameeleza kuwa badala ya kuhamasisha umoja, kampeni hiyo inazua migawanyiko isiyo ya lazima ndani ya CHADEMA.

Akiwasihi wanachama wa CHADEMA katika Tunduma, Elisha amewataka kupuuza siasa za upendeleo na kuzingatia maslahi ya chama kwa ujumla. Amesisitiza kuwa siasa safi ni zile zinazojenga mshikamano, sio zinazotengeneza makundi na misuguano isiyo na tija.

#WanaTukutaneOktoba2025

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *