Mzee Shila Hailele Mponda, mkazi wa Jimbo la Tunduma, ameibua hoja nzito dhidi ya kampeni ya “No Reforms No Election” inayoendeshwa na kikundi cha Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Mzee Shila ameeleza kuwa tayari wanasiasa wa CHADEMA kutoka jimbo lao, akiwemo aliyekuwa Mbunge Frank Mwakajoka na mwanasiasa kijana Boniface Mwakabanje, wameshatangaza nia ya kugombea ubunge.
Amesema kuwa kikundi cha Tundu Lissu kinachopinga uchaguzi hakina mvuto wala uungwaji mkono katika Jimbo la Tunduma, kwani wananchi wanaelewa kuwa uchaguzi ni haki ya kikatiba.
Kwa mujibu wa Mzee Shila, hakuna mtu au kikundi kinachopaswa kuzuia raia yeyote kugombea ifikapo mwezi Oktoba, kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoelekeza.
Kwa msingi huo, Mzee Shila amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchaguzi mkuu haucheleweshwi wala kusitishwa kwa sababu ya shinikizo au kelele za kisiasa kutoka kwa kundi lolote, bali uendelee kama ilivyopangwa kikatiba.
#sisinitanzania #MSLAC #Katibanasheria #Tanzania
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+