ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ina Mchango Mkubwa katika Mipango na Sera za kuendeleza Uchumi wa Buluu unaozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za Bahari

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi Jengo la Taaluma na Utawala la taasisi hiyo Buyu ,Wilaya ya Magharibi B ,Mkoa wa Mjini Magahribi. Aidha Rais Mwinyi ameahidi Serikali kuendelea Kushirikiana na Taasisi hiyo wakati wote kwa lengo la kuhakikisha Rasilimali za Bahari ziliyopo zinatumika ipasavyo ili kutoa Mchango …

Soma zaidi »

“LEO DISEMBA 31, 2024 MWISHO MATUMIZI YA KUNI NA MKAA KWA TAASISI ZA UMMA”- MAJALIWA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amezikumbusha Taasisi na mashirika yote ya Serikali yaliyopo kote nchini Tanzania ambayo yanahudumia watu zaidi ya 100, kutekeleza bila shuruti agizo lake la kuitangaza Disemba 31, 2024 kuwa siku ya mwisho kwa matumizi ya Mkaa na Kuni kwenye …

Soma zaidi »

Kheri ya siku ya kumbukizi Miaka 25 toka kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Tuendelee kuenzi Matokeo chanyA+ ya juhudi zake za kujenga umoja, amani, na maendeleo kwa taifa letu. Umoja ni nguvu, tukumbuke daima mafunzo yake kwa mustakabali wa Tanzania iliyo bora. #KaziIemdelee#SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu#SSH#CCM#KaziIendelee#Nchiyangukwanza#SisiniTanzania#matokeochanya#MSLAC

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar wakati akitokea Harare nchini Zimbabwe

Mhe. Rais Dkt. Samia alishiriki Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya hiyo (SADC-Organ Troika)

Soma zaidi »