VIJANA WA NKASI WAJITOKEZE KWA WINGI UCHAGUZI MKUU 2025 – JUSTINE JANUARI KIBOKO.

Justine Januari Kiboko, mkazi wa Namanyere, Kata ya Majengo, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, ametoa wito kwa vijana wote wa Nkasi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025.

Amesema vijana ni nguvu kazi ya taifa na wanayo nafasi kubwa ya kuamua mustakabali wa nchi kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Ameongeza kuwa madai mengi yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya vyama vya upinzani yameshughulikiwa na serikali, ikiwemo kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuondolewa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi.

Kwa msingi huo, Kiboko amesema hakuna sababu yoyote ya wananchi wa Nkasi kususia uchaguzi au kuyumbishwa na kundi dogo lenye maslahi binafsi ya kuleta machafuko nchini.

Amewahimiza wananchi kushiriki uchaguzi bila kujali itikadi zao za kisiasa, kwani maendeleo hayabagui chama bali yanakuja kupitia uchaguzi wa viongozi bora.

Kiboko amehitimisha kwa kusema kuwa ni jukumu la kizalendo kwa kila kijana kujitokeza na kupiga kura kwa amani na utulivu ili kuendeleza amani na maendeleo ya Taifa.

#SisiNiTanzania #MSLAC #Haki

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *