Askofu Mstaafu Ambele Mwaipopo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Rukwa, amepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza maridhiano ya kitaifa na kusukuma mbele maendeleo ya nchi.
Amesema moja ya mafanikio makubwa yanayoonekana mkoani Rukwa ni kuunganishwa kwa Jiji la Sumbawanga kupitia mtandao wa barabara za kisasa, jambo ambalo limerahisisha sana usafiri na kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa huo.
Askofu Mwaipopo ameongeza kuwa Jumuiya ya Maridhiano na Amani inatambua kwa dhati mchango wa Rais Samia katika kulinda na kuimarisha umoja wa kitaifa kupitia maridhiano, upendo na ushirikiano baina ya Watanzania wa kada zote.
Amesisitiza kuwa ni muhimu maridhiano yaheshimiwe na kudumishwa kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Jumuiya hiyo inaendelea kuiombea serikali iendelee kudumu katika amani, na uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 uwe wa utulivu, haki na ushiriki mpana wa wananchi wote kwa njia ya amani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
#sisinitanzania #maendeleo #tanzaniampya #sisinitanzaniampya #tanzaniayetu #tanzanianamaendeleo #tanzania #samiasuluhu #ssh #sisinitanzaniamakini #sisinitanzania #tanzaniabora #millardayo #updates #news #habari #habarimpya
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+