NI WAKATI WA KUIMARISHA AMANI KWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025: MCHUNGAJI FIDELISI MAHEKE, NKASI.

Mchungaji Fidelisi Maheke ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Agape Life Wilaya ya Nkasi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste na Katibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania katika Wilaya ya Nkasi, ametoa wito wa kuhimiza amani, mshikamano na ushiriki wa wananchi katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Amesema kuwa mwaka 2025 ni mwaka muhimu kwa Watanzania wote, kwani ndiyo utakaowapa fursa ya kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani watakaosimamia maendeleo ya taifa.

Hata hivyo, ameeleza kwa masikitiko kuwepo kwa watu wanaozunguka mitaani wakipinga kufanyika kwa uchaguzi, jambo alilolieleza kuwa ni jaribio la kukwamisha maendeleo ya Wilaya ya Nkasi na nchi kwa ujumla.Akinukuu Waraka wa Kwanza wa Timotheo 2:1-3, Mchungaji Maheke amesema Biblia inasisitiza umuhimu wa sala, dua, amani na utulivu kwa ajili ya viongozi.

Hivyo, kushiriki katika uchaguzi ni njia mojawapo ya kutekeleza wajibu huo wa kiroho na kijamii.Amehimiza wananchi wa Nkasi kupuuza maneno ya upotoshaji na badala yake waungane kwa mshikamano na amani, wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi ili kuchagua viongozi wa kuendeleza taifa.

#WanaTukutaneOktoba2025

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *