Mzee Edward Peter Maganga ametoa wito kwa vijana wa Tanzania kusimama imara kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vitendo, hasa kwa kulinda amani na utulivu wa nchi.
Amesema maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa yametokana na kuheshimu utaratibu, sheria na misingi ya kidemokrasia ambayo imeijenga Tanzania kuwa taifa lenye mshikamano.
Maganga amehoji kwa mshangao ni vipi mtu anaweza kutamka hadharani kwamba hakuna uchaguzi, jambo ambalo ni tishio kwa usalama wa taifa. Amesema kauli kama hizo zinapaswa kupingwa vikali na vijana wote, kwani zina nia ovu ya kuvuruga amani na maendeleo ya nchi.
Amewasihi vijana wa Tanzania kusimamia nchi yao kwa moyo wa kizalendo, kulinda utulivu na kuhakikisha uchaguzi mkuu wa 2025 unafanyika kwa amani, ushiriki mpana na kwa heshima ya taifa.
#sisinitanzania #tanzania #mslac #katibanasheria #nchiyangukwanza #kaziiendelee #matokeochanya #ssh #ccm #bungelive
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+