Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa nchi imefanikiwa kuondoa njaa kwa asilimia 100, huku ikijitosheleza kwa chakula kwa asilimia 128.
Akizungumza kuhusu hali ya usalama wa chakula nchini, Rais Samia alibainisha kuwa mafanikio haya yanatokana na jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali katika sekta ya kilimo, ikiwemo uwekezaji katika mbegu bora, umwagiliaji, na uboreshaji wa masoko ya mazao.
“Tumeshaondoa njaa kwa asilimia 100. Na katika lengo la kujitegemea kwa chakula, Tanzania tunajitegemea kwa asilimia 128. Sasa kilichobaki ni mtu mmoja mmoja na jitihada zake kuhakikisha habaki na njaa au halali na njaa,” alisema Rais Samia.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kuhakikisha anatumia fursa zilizopo ili kujihakikishia chakula cha kutosha kwa kaya yake. Serikali kwa upande wake inaendelea kuimarisha miundombinu ya kilimo na usambazaji wa pembejeo ili kuhakikisha uzalishaji wa chakula unaendelea kuongezeka.
Mafanikio haya yanathibitisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na usalama wa chakula wa kutosha, huku wananchi wakihimizwa kuongeza uzalishaji kwa maendeleo endelevu ya taifa.”
#sisinitanzania #mslac #katibanasheria #matokeochanya #ssh #nchiyangukwanza #nchiyangukwanza #tanzania #ccm #bungelive
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+