Eunice Isaack Wilomo amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu, hususan kuendeleza elimu bila malipo kwa watoto wa Kitanzania. Amesema serikali ya Awamu ya Sita imeboresha mazingira ya kujifunzia kwa kuweka umeme mashuleni, kuweka madirisha ya kisasa na marumaru kwenye madarasa, jambo linalochochea ubora wa elimu katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Sumbawanga.
Ameeleza kuwa wananchi wa Sumbawanga wanatambua na kuthamini jitihada hizo, na wako tayari kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu, bila kwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5(1) ya Katiba, kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi ana haki ya kupiga kura katika uchaguzi. Eunice amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila raia kuheshimu ibara hii kwa kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi watakaoendeleza mafanikio yaliyopo.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+