TUILINDE AMANI KWA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025

Ibrahim Hamisi Msaga, mkazi wa Manispaa ya Sumbawanga kata ya Katandala, ameipongeza serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika Mkoa wa Rukwa. Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege, Hospitali za kisasa, na shule zenye miundombinu bora inayoboresha elimu ya watoto wa Kitanzania.

Amesema mafanikio haya ni matokeo ya uongozi wenye dira na mshikamano, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda amani na kuyathamini maendeleo yaliyopatikana. Msaga amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 kama njia ya kulinda katiba na haki ya kidemokrasia.

Amesisitiza kuwa wale wanaohamasisha kugomea uchaguzi hawana nia njema na taifa, hivyo ni muhimu kupingwa na kukataliwa kwa nguvu zote. Amani ni nguzo ya maendeleo, na kila mmoja ana jukumu la kuilinda kwa vitendo.

#WanaTukutaneOktoba2025

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *