TUMETESEKA KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA UHABA WA MAJI, LAKINI SASA TUNA HAKIKA YA KUPATA MAJI SAFI.

“Tumeteseka kwa muda mrefu kutokana na uhaba wa maji, lakini sasa tuna hakika ya kupata maji safi na salama. Tunamshukuru sana Rais Samia kwa kutuletea maendeleo haya,” alisema Mariam Salum, mkazi wa Same.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameuzindua rasmi Mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe, hatua inayotarajiwa kuondoa changamoto ya uhaba wa maji kwa maelfu ya wananchi katika wilaya hizo.

Mradi huu mkubwa, ambao unategemea maji kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu, unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wananchi 456,931 kutoka wilaya za Same, Mwanga, na Korogwe. Mradi huu pia unajumuisha mtambo wa kisasa wa kutibu maji uliopo wilayani Mwanga, ambao utahakikisha maji yanapatikana kwa usafi na ubora wa hali ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia alisema kuwa mradi huu ni sehemu ya juhudi za serikali kuhakikisha huduma bora za maji zinawafikia wananchi kwa wakati, huku akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika miradi ya maji vijijini na mijini.

#sisinitanzania #mslac #katibanasheria #matokeochanya #nchiyangukwanza #nchiyangukwanza #ssh #kaziiendelee #tanzania #tanzania #ccm #bungelive

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *