Kilimanjaro, Tanzania – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa Mamlaka ya Maji mkoani Kilimanjaro kuhakikisha wanaharakisha utoaji wa huduma kwa wananchi ili wasikose huduma hiyo muhimu.
Aidha, Rais Samia amesisitiza kuwa mamlaka hiyo ihakikishe huduma ya maji haikatwi katika siku za sikukuu na mwisho wa wiki, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa usambazaji endelevu wa maji safi na salama kwa wananchi.
Mradi wa maji wa Same – Mwanga – Korogwe unalenga kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Tanga, hatua inayotarajiwa kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Ziara ya Rais Samia katika mkoa wa Kilimanjaro inadhihirisha dhamira yake ya kuboresha huduma za maji nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wananchi wote.
#sisinitanzania #mslac #katibanasheria #matokeochanya #nchiyangukwanza #ssh #kaziiendelee #ccm #bungelive
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+