MAKONDA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA, ATOA WITO KWA TLS KUJITOKEZA ZAIDI!

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Makonda, amepongeza juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha na kuendeleza kampeni ya msaada wa kisheria kwa wananchi, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, hususan kwa makundi yenye uhitaji mkubwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makonda ameiomba Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kushiriki kikamilifu katika kampeni hii kwa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi, kusaidia uelewa wa haki zao, na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki bila vikwazo vya kiuchumi au kijamii.

#AsanteRais #HakiKwaWote #MsaadaWaKisheria #TLS #Arusha

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *