RAIS SAMIA KAZINDUA SERA MPYA YA TAIFA YA ARDHI: MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU

DODOMA, 17 Machi 2025 – Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center umejaa viongozi na wageni mashuhuri, wakishuhudia tukio la kihistoria – uzinduzi rasmi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995, Toleo la 2023. Hafla hii muhimu inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye mgeni rasmi.

Uzinduzi huu, unaobeba kaulimbiu “Sera ya Ardhi – Msingi wa Ustawi na Maendeleo Endelevu ya Taifa”, unaashiria hatua kubwa katika kusimamia, kulinda, na kuendeleza rasilimali za ardhi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Viongozi wa kitaifa, wataalamu wa ardhi, wabunge, wawakilishi wa sekta binafsi, pamoja na wadau wa maendeleo wamekusanyika kushuhudia mapinduzi haya ya sera yanayolenga kuimarisha usimamizi wa ardhi kwa ustawi wa taifa.

Kwa miaka mingi, changamoto katika sekta ya ardhi zimekuwa kikwazo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Hata hivyo, kupitia sera hii mpya, Tanzania inalenga kutatua masuala ya umiliki wa ardhi, mabadiliko ya matumizi ya ardhi, na kuhakikisha uwekezaji endelevu unaoleta maendeleo kwa wananchi wote.

Hotuba ya Rais Samia inatarajiwa kutoa dira na mwelekeo mpya wa usimamizi wa ardhi, ikisisitiza umuhimu wa matumizi bora ya ardhi kama nyenzo kuu ya maendeleo ya taifa.

Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi kuhusu mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kupitia sera hii mpya ya ardhi!

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *