Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu kwaniaba ya Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo Machi 17, 2025 amesema ndani ya miezi minne ya Rais Samia Suluhu Hassan mambo mengo yaliyokuwa yameshindikana yamefanyika ikiwemo maandalizi na uzinduzi wa sera ya Ardhi ya mwaka 1995, toleo la mwaka 2023.
Wakati wa Uzinduzi wa sera hiyo unaofanywa na Rais Samia Mjini Dodoma kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, Mhe. Zungu amesema kuzinduliwa kwa sera hiyo kutadumisha na kuimarisha amani ya Tanzania kwani migogoro ya ardhi na mivutano kati ya wakulima na wafugaji inaenda kuhitimishwa kwa kuimarisha na kutoa haki ya ardhi kusimamiwa kikamilifu kwa watanzania.
Katika salamu zake fupi kwaniaba ya Mhe. Tulia anayehudhuria Mkutano wa Mabunge duniani, Mhe. Zungu pia amewasihi watendaji mbalimbali wa sekta ya ardhi nchini kusimamia sekta hiyo kikamilifu katika kuhakikisha kuwa inakuwa na mchango mkubwa kwenye pato la serikali kutokana na umuhimu mkubwa wa rasilimali hiyo yenye kupanda thamani kila wakati.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+