Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Ayasi Njalambah, amesisitiza kuwa amani na utulivu ni fahari ya Jiji la Mbeya na msingi wa maendeleo endelevu.
Sheikh Njalambah amepongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kujenga jamii yenye umoja na mshikamano, akisema kuwa serikali imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanaishi kwa upendo na maridhiano.
Aidha, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa nchi moja yenye mshikamano wa kitaifa. Ametaja kuwa hatua ya kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ni matokeo ya maridhiano ya pamoja kati ya wadau mbalimbali wa siasa, jambo ambalo linaimarisha demokrasia nchini na kuleta matumaini ya uchaguzi huru na wa haki mwaka 2025.
Sheikh Njalambah pia amekemea vikali wale wote wanaopanga kusababisha vurugu au kujaribu kuwazuia wananchi wa Mbeya kushiriki katika mchakato wa uchaguzi. Amesisitiza kuwa kila Mtanzania ana haki ya kidemokrasia ya kujiandikisha na kupiga kura bila hofu.
Amewataka wananchi wa Mbeya kudumisha amani na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ili kuendeleza maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla na kupuuza wanasiasa wenye nia ya kuwagawa na kusababisha mpasuka katika jamii.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+