Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Barbados, Mhe. Mia Mottley ambapo wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili

Mazungumzo hayo yamefanyika katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mia Mottley, Jijini Bridgestone, nchini Barbados.

Waziri Mkuu Mia amesema, kuna umuhimu wa kuwa na mkakati wa pamoja na kushirikiana kwa lengo la kukuza utalii kati ya Barbados na Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla. Amesema kuna maeneo mengi ya vivutio vya utalii ambavyo vinaweza kuzinufaisha pande hizo mbili yakiwemo masuala ya ukarimu.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni katika utoaji wa mafunzo maeneo ya ufundi kati ya nchi za Carib (Caribbean) na nchi mbalimbali za kiafrika huku akisisitiza kuwa umuhimu wa uboreshaji wa masoko na kubadilishana wataalam katika sekta mbalimbali kwa makubaliano maalum.

Aidha, amesema upo uhitaji wa wataalam katika sekta ya maji na miundombinu na hivyo kuna uwezekano wa kubadilishana wataalam ili kujengeana uzoefu katika sekta mbalimbali kulingana na makubaliano yatakayofikiwa.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *