ZAIDI YA WATU LAKI NNE KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI ARUSHA

Arusha, Machi 1, 2025 – Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian, ametangaza kuwa zaidi ya watu laki nne wanatarajiwa kushiriki katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mhe. Maximilian amesema maandalizi yanaendelea vizuri, huku jiji likijiandaa kupokea wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania. “Maadhimisho haya ni fursa muhimu ya kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa letu. Tumeshuhudia jitihada za wanawake katika sekta mbalimbali, na siku hii ni ya kusherehekea mafanikio yao,” alisema.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *