CHIFU – ROCKETI MASOKO MWANSHINGA , AKEMEA WANAOPANGA KUZUIA WANANCHI KUJITOKEZA KWENYE UCHAGUZI.

Chifu wa Mkoa wa Mbeya, Rocketi Masoko Mwanshinga, amewataka wananchi wote wa mkoa huo kutumia haki yao ya kikatiba kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Chifu Mwanshinga amekemea vikali wale wote wanaotaka kuwazuia wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi, akisema Mungu atawapa usingizi na hawataweza kuzuia uchaguzi kufanyika.

Amesisitiza kuwa kila raia ana haki ya kupiga kura na kupigiwa kura bila hofu wala vizuizi vyovyote. Aidha, Chifu Mwanshinga amemuombea Rais Samia Suluhu Hassan apate ushindi wa kishindo, akisema kuwa uongozi wake umekuwa wa neema kwa Watanzania.

Amewataka wakazi wa Mbeya kuungana kwa mshikamano na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao wa kidemokrasia ili kuchagua viongozi watakaosukuma mbele maendeleo ya Tanzania.

#WanaTukutaneOktoba2025 #MbeyaYaKijani #KaziNaUtuTunasongaMbele #SisiniTanzania #Nchiyangukwanza #MSLAC

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *