Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, Machi 21, 2025 amewasili Mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Siku ya Misitu Duniani inayofanyika kitaifa Mkoani Njombe

Akiwa Mkoani humo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ametembelea kiwanda cha uchakataji mazao ya misitu cha TANWAT (Tanganyika Wattle Company Limited) kilichopo Njombe mjini ambapo ameshuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.

Akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa kiwanda hicho kufanya kazi kwa weledi ili kufanikisha malengo ya muwekezaji.

“fanyeni kazi kwa uaminifu, fanyeni kazi kwa uadilifu, na kwa weledi”.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *