Ushirikiano wa Wananchi na Serikali katika Kuboresha Huduma za Afya

Kituo cha Afya Kafita, kilichopo katika Wilaya ya Nyang’hwale, Kata ya Kafita, kijiji cha Kafita, ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya wananchi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na serikali kuu. Ujenzi wa kituo hiki umegharimu jumla ya shilingi milioni 200, fedha ambazo zilitokana na juhudi za wananchi, msaada wa TASAF, na mchango mkubwa wa serikali kuu.

Kituo hiki kilianza kutoa huduma mwishoni mwa mwaka 2023 na kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo. Huduma zinazotolewa zimeimarisha upatikanaji wa matibabu ya msingi kwa jamii, hivyo kupunguza changamoto za kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma za afya.

Ujenzi wa kituo hiki unaakisi dhamira ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha sekta ya afya kwa kushirikiana na wananchi. Wakazi wa Kafita sasa wanapata huduma bora za afya karibu na makazi yao, hatua inayochangia kuboresha ustawi wa jamii kwa ujumla. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @IkuluMawasiliano

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *