Pichani, Waziri Mkuu akizungumza na Brightina Francis wa kijiji cha Gendabi baada ya kuzindua nyumba hizo zilizojengwa katika kitongoji cha Waret wilayani humo
Soma zaidi »Maktaba ya Kila Siku: December 20, 2024
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud kufuatia mwaliko wa Rais huyo yaliyofanyika katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Mogandishu
Viongozi hao wameelezea kuhusu dhamira yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi kati ya mataifa hayo mawili. Waziri Kombo yupo nchini Somalia kwa ziara ya kikazi ambapo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya kutia saini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Jamhuri ya …
Soma zaidi »Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kuaga mwili wa marehemu John Billy Tendwa ambaye aliwahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Akitoa Salama pole kwa waombolezaji wakati wa tukio la kuaga lililofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kuyaenzi mema yote aliyoyafanya marehemu Tendwa katika kipindi cha uhai wake. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Marehemu Tendwa …
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+