Kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Igava kilichopo Kijiji cha Igunda Muungano, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, inaendelea kwa kasi. Ujenzi huu unafadhiliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400, zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Fedha hizi ni sehemu ya juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya vijijini, kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora karibu na makazi yao. Kituo hiki cha afya kinatarajiwa kupunguza changamoto za huduma za afya katika eneo hilo, kwa kuleta huduma karibu na wananchi wa Kata ya Igava na maeneo jirani.
Kwa sasa, hatua mbalimbali za ujenzi zinaendelea, zikiwemo ujenzi wa majengo muhimu ya kituo hicho. Wananchi wa eneo hilo wameonesha kuridhika na juhudi hizi za serikali, wakiamini kuwa ujenzi wa kituo hicho utachochea maendeleo ya kijamii na kuboresha ustawi wa maisha yao.
Huu ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha maendeleo ya sekta ya afya yanafikiwa katika kila kona ya nchi. #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+