Katika juhudi za kuhakikisha haki inawafikia wananchi wa kila kona ya Tanzania, huduma ya msaada wa kisheria sasa imeimarishwa kwa kupata usafiri wa kisasa. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kupanua wigo wa huduma za kisheria kwa wananchi wote, hususan wale wa maeneo ya vijijini na walio katika mazingira magumu.
Kwa kutumia vyombo vya usafiri vilivyotolewa, mawakili na watoa huduma wa msaada wa kisheria wataweza kufika maeneo ya mbali ambayo awali yalikuwa changamoto kufikiwa. Hatua hii itawawezesha wananchi wengi zaidi kupata msaada wa kisheria, elimu kuhusu haki zao, na usaidizi wa kufungua mashauri yao kwa wakati. #MSLAC. #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+