Wamekutana na kuzungumza kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza (27.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano wa katika kuboresha miundombinu nchini, ukiwemo Mradi wa …
Soma zaidi »Maktaba ya Kila Siku: January 27, 2025
Rais wa Burundi Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye, alipowasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati
Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye yuko nchini kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaowakutanisha Viongozi wa Nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la …
Soma zaidi »Rais wa Malawi, Dk Lazarus Chakwera, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati
Mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo Januari 27 hadi kesho Januari 28, 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo alilakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Saada Mkuya, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano …
Soma zaidi »Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama amewasili jijini Dar es Salaam Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
Mhe. Mahama amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na …
Soma zaidi »RAIS WA ZAMBIA AWASILI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA MKUTANO WA NISHATI
Rais wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema, amewasili jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika nchini kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, …
Soma zaidi »Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Taasisi ya Rockefeller Dkt. Rajiv Sha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohamed
RAIS WA MAURITANIA AWASILI TANZANIA KWA AJILI YA MKUTANO WA NISHATI
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, Mheshimiwa Mohamed Ould Ghazouani, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati. Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Mohamed Ould Ghazouani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa …
Soma zaidi »Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mhe. Dkt. Doto Biteko katika mkutano wa Mawaziri wa Nishati na Fedha barani Afrika
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua Mkutano wa Mawaziri wa Nishati na Fedha barani Afrika ambao umehusisha Wadau wa Maendeleo wakiongozwa na Rais wa Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo Afrika. Mkutano huo ni sehemu ya Mkutano wa #Mission300
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+