Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu (Asian Infrastructure Investment Bank – AIIB), Bw. Jin Luqun

Wamekutana na kuzungumza kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza (27.01.2025), katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano wa katika kuboresha miundombinu nchini, ukiwemo Mradi wa kimkakati wa Reli ya Kisasa (SGR).

Kikao hicho kiliwashirikisha pia Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Benki hiyo.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *