
Mheshimiwa Evariste Ndayishimiye yuko nchini kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaowakutanisha Viongozi wa Nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo.


Mkutano huo unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+