

Mkutano huo unafanyika nchini kuanzia leo Januari 27 hadi kesho Januari 28, 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo alilakiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dk Saada Mkuya, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, na maofisa waandamizi wa Serikali