Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama amewasili jijini Dar es Salaam Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaoendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere

Mhe. Mahama amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Hamidu Aweso.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo.

Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalodhamiria kuimarisha juhudi za pamoja za Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika katika kuhakikisha Afrika inaondokana na changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu.



Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *