Hayo yameelezwa Desemba 11, 2024 Jijini Dodoma na NaibuKatibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Christina Mndeme wakati wa mazungumzo baina yake naUjumbe wa Wizara ya Maliasili na Mabadiliko ya Tabianchiwa Serikali ya Jamhuri ya Malawi ulioongozwa naMkurugenzi wa Mazingira wa Wizara hiyo, Bi. TawongaMbale-Luka.

Mndeme amesema mataifa mbalimbali kwa sasa yanakabiliwana athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ongezeko la joto, mvua zisizotabirika na mabadiliko ya mifumo ya hali yahewa na hivyo kuhitajika kwa nguvu za pamoja zakukabiliana ikiwemo kuimarisha ushirikiano wa kikandabaina ya mataifa.
Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua umuhimuwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa katika kukabiliana naathari za mabadiliko ya tabianchi ambapo Tanzania imeridhiamikataba mbalimbali ya Mabadiliko ya Tabianchi, Itifaki yaKyoto na Makubaliano ya Paris.

“Jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi zimeibuachangamoto na fursa muhimu ambazo zinaweza kusaidiaTanzania katika kuchochea uhifadhi wa mazingira namaendeleo endelevu ikiwa ni pamoja na kufanya mapitio yasera, uandaaji wa kanuni, mikakati na miongozo” amesemaMndeme.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+