Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Mhe. Hamfrey Polepole, ameeleza jinsi Watanzania watakavyonufaika na matibabu ya magonjwa adimu kutoka Cuba. Tayari dawa za magonjwa hayo zimewasili nchini na kusambazwa kwenye mojawapo ya hospitali. Mpango huu utaimarisha huduma za afya na kuhakikisha tiba za kisasa kwa magonjwa kama kansa na kisukari zinapatikana.