NILITAMANI KUFA MARA MOJA KULIKO MATESO YALE YA POLEPOLE

Mraibu wa dawa za kulevya anaeleza kwa uchungu jinsi alivyotamani dawa hizo zingekuwa ni sumu ya kumuua alipokuwa akizitumia, badala ya kumwacha hai ili aendelee kuteseka.

Anasema mateso aliyoyapitia kwa zaidi ya miaka 15 yalikuwa makubwa kuliko maumivu ya kifo alikosa amani, heshima, kazi, familia na afya.

Kila alipozitumia alitamani iwe mara ya mwisho, lakini utegemezi ulimweka kifungoni.

Leo hii, akiwa katika safari ya kupona, anawasihi wengine waepuke kabisa, akisema: “Nilitamani bora kufa mara moja kuliko mateso yale ya polepole.”

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

Mwisho.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *