ONA USHIRIKIANO MADHUBUTI WA JESHI LA POLISI NA DCEA KATIKA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa taifa salama na lenye watu wenye afya bora na maadili mema, Jeshi la Polisi limeimarisha ushirikiano wake na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) katika jitihada za kuzuia, kubaini na kutokomeza kabisa matumizi na biashara ya dawa za kulevya nchini.

Kupitia kitengo maalum cha Anti-Drugs Unit (ADU), Jeshi la Polisi limekuwa likishirikiana na DCEA katika oparesheni za kitaifa ambazo zinajumuisha ukamataji wa watuhumiwa, uteketezaji wa dawa haramu na upelelezi wa kina katika kanda zote zilizoundwa na mamlaka hiyo. Wakuu wa upelelezi wa makosa ya jinai pia wamepewa maelekezo maalum ya kushirikiana kwa karibu na DCEA ili kuhakikisha mtandao wa usambazaji wa dawa hizo unavunjwa kwa ukamilifu.

Aidha, Jeshi la Polisi limekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa jamii kwa kuonesha kwa uwazi sampuli za dawa hizo haramu ili wananchi wazitambue, waweze kutoa taarifa, na kuchukua tahadhari mapema. Dawa hizo ni pamoja na heroin, cocaine, bangi, mirungi, methamphetamine, nk

Ushirikiano huu madhubuti unalenga kujenga jamii inayotambua hatari za dawa za kulevya na kujiwekea kinga dhidi ya janga hili, huku serikali ikidhamiria kuacha historia mpya isiyo na nafasi kwa biashara na matumizi ya dawa hizo hatari.

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

#DCEA #OktobaTunatiki

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *