Mdau wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya Nuru Saleh Ahmed ameeleza kuwa Ni muhimu kwa Serikali kushirikiana na jamii katika kuwawezesha waraibu wa zamani wa dawa za kulevya kwa kuwapatia mitaji na fursa za kiuchumi baada ya wao kuacha matumizi ya dawa hizo. Utafiti na hali halisi unaonesha kuwa wengi hurudia matumizi ya dawa za kulevya si kwa sababu ya tamaa, bali kwa kukosa shughuli za kuwapatia kipato, hali inayowarudisha kwenye mazingira yale yale yaliyowachochea kutumia awali.
Kwa kuwapatia mitaji midogo, mafunzo ya ujasiriamali na ufuatiliaji wa karibu, waraibu hawa wanaweza kuanzisha shughuli halali zitakazowapatia kipato na kuwaepusha na kurudi katika utegemezi. Baadhi ya shughuli wanazoweza kujishughulisha nazo ni pamoja na ufugaji wa kuku, nguruwe au mbuzi, kilimo cha mbogamboga, useremala, ushonaji wa nguo, biashara ndogo ndogo kama kuuza matunda, vinywaji baridi au chakula; na kazi za sanaa kama uchoraji au muziki.
Uwezeshaji huu si tu unawasaidia wao binafsi, bali pia unachangia usalama wa jamii, kupunguza uhalifu unaotokana na utegemezi wa dawa za kulevya, na kuongeza nguvu kazi katika maendeleo ya taifa. Serikali na jamii zikisimama pamoja, mabadiliko chanya yanawezekana.
Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”
Mwisho.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+