TUJITOKEZE KWA WINGI! TUUNGANE NA RAIS SAMIA KATIKA KILELE CHA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Wana-Dodoma na Watanzania kwa ujumla, mnakaribishwa kushiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Matumizi na Biashara ya Dawa za Kulevya kitakachofanyika tarehe 26 Juni 2025, kuanzia saa 1:00 asubuhi, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, Dodoma.

Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukio hili litatumika kutoa elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa jamii na taifa. Jitokeze kwa wingi – Tuijenge Tanzania isiyo na dawa za kulevya!

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *