CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI KIGAMBONI: NGUVU MPYA KATIKA KUINUA MAISHA NA UJUZI WA JAMII

Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Kigamboni (FDC-KIGAMBONI), kilichozinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023, ni mradi muhimu wa maendeleo ya kijamii unaolenga kuinua maisha ya wananchi kwa kuwapatia elimu ya vitendo na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na shughuli za kiuchumi. Chuo hiki ni sehemu ya juhudi za serikali za kuhakikisha maendeleo shirikishi na endelevu kwa jamii za Kigamboni na maeneo jirani.

Lengo na Umuhimu wa Chuo

Lengo kuu la FDC-Kigamboni ni kutoa mafunzo ya kiufundi na ya vitendo yanayolenga kuboresha ustawi wa kiuchumi na kijamii wa wananchi. Chuo hiki kinatambua umuhimu wa elimu ya vitendo katika kuboresha maisha, kuongeza ajira, na kuimarisha uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla. Kwa kufundisha maarifa ya kisasa na yanayohusiana moja kwa moja na mahitaji ya soko, chuo kinasaidia kuziba pengo la ujuzi kati ya vijana wasio na ajira na fursa zilizopo.

Unaweza kuangalia pia

NEMC YAZINDUA RASMI KAMPENI YA ‘NEMC USAFI KAMPENI’

Oni moja

  1. Mimi naitwa FADHILI MSUYA Nina miaka 24, pia ni muhitimu wa Shahada ya Utawala kwa Umma yaani PUBLIC ADMINISTRATION kutoka chuo kikuu Mzumbe mkoani MOROGORO, pia Nina Astashada na Stashaada ya COMMUNITY DEVELOPMENT kutoka chuo cha maendeleo ya Jamii UYOLE-MBEYA. Naomba kujitolea kufundisha kwani ninauwezo mzuri wa kufundisha.
    LOCATION: DARESALAAM
    TAFADHALI NISAIDIENI
    0656567442
    [email protected]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *