MatokeoChanya

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MWENDOKASI AWAMU YA NNE WAENDELEA KWA KASI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) awamu ya nne, ikiwa ni juhudi za kuboresha usafiri wa umma jijini Dar es Salaam. Awamu hii inahusisha ujenzi wa njia kuu ya mwendokasi yenye urefu wa kilometa 13.5, inayotoka …

Soma zaidi »

HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA YAPATA USAFIRI KUWAFIKIA WANANCHI WENGI ZAIDI

Katika juhudi za kuhakikisha haki inawafikia wananchi wa kila kona ya Tanzania, huduma ya msaada wa kisheria sasa imeimarishwa kwa kupata usafiri wa kisasa. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kupanua wigo wa huduma za kisheria kwa wananchi wote, hususan wale wa maeneo ya vijijini na walio katika mazingira …

Soma zaidi »

Ijumaa, Desemba 20, 2024, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi rasmi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Nyumba hizo zimejengwa katika kitongoji cha Waret, Hanang, ikiwa ni juhudi za Serikali kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika na kuimarisha ustawi wao

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwasaidia. “Ujenzi huu ni ishara ya upendo na kujali kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, aliyetoa maelekezo ya kujenga nyumba bora na za kudumu kwa …

Soma zaidi »

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mheshimiwa Dkt. Hassan Sheikh Mohamud kufuatia mwaliko wa Rais huyo yaliyofanyika katika Ikulu ya Nchi hiyo jijini Mogandishu

Viongozi hao wameelezea kuhusu dhamira yao ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi kati ya mataifa hayo mawili. Waziri Kombo yupo nchini Somalia kwa ziara ya kikazi ambapo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya kutia saini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Jamhuri ya …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 19, 2024 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kuaga mwili wa marehemu John Billy Tendwa ambaye aliwahi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Akitoa Salama pole kwa waombolezaji wakati wa tukio la kuaga lililofanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa wanafamilia, ndugu na waombolezaji kuyaenzi mema yote aliyoyafanya marehemu Tendwa katika kipindi cha uhai wake. Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Marehemu Tendwa …

Soma zaidi »

TANZANIA NA OMANI ZASAINI MKATABA WA KUTOTOZA KODI MARA MBILI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kisultan ya Oman, zimetia saini Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi ya Mapato Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji Kodi, ujulikanao kama Agreement for the Elimination of Double Taxation with Respect to Taxes on Income and Prevention of Tax Avoidance and Evasion. …

Soma zaidi »

Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayosimamia kada ya Ununuzi na Ugavi nchini.

Mhe. Dkt. Biteko alisema kuwa Sekta ya Ununuzi na Ugavi ndio eneo pekee linalochukua takribani asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali, hivyo uadilifu pekee ndio utakaosaidia fedha kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa hasa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri …

Soma zaidi »

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni awasili katika Ofisi ndogo ya Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo Desemba 16,2024, baada ya kuteuliwa hivi karibuni

Waziri Masauni amepokelewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Soma zaidi »

DKT. NCHEMBA AHIMIZA USHIRIKIANO WA KIKODI NA OMAN

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza katika kikao kifupi na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mapato ya Oman, Bw. Nasser Khamis Al-Jashmir, kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Oman na Tanzania katika eneo la kodi ili kurahisisha ufanyaji biashara kwa faida ya nchi hizo mbili. …

Soma zaidi »