MAJANGA

Ijumaa, Desemba 20, 2024, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekabidhi rasmi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Nyumba hizo zimejengwa katika kitongoji cha Waret, Hanang, ikiwa ni juhudi za Serikali kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika na kuimarisha ustawi wao

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na kusisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwasaidia. “Ujenzi huu ni ishara ya upendo na kujali kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, aliyetoa maelekezo ya kujenga nyumba bora na za kudumu kwa …

Soma zaidi »