MatokeoChanya

Ongezeko la uchumi wa Tanzania limeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali, lakini tunataka kusikia kutoka kwako! Je, unadhani ongezeko hili linachangia katika kuboresha maisha ya wananchi?

Gusa link hapo chini tuendelee kuelimika zaidi https://matokeochanya.blogspot.com/2024/12/je-ongezeko-la-uchumi-wa-tanzania.html…#MSLAC#Katibanasheria#SSH#CCM#KaziIendelee#Nchiyangukwanza#SisiniTanzania#matokeochanya @samia_suluhu_hassan @IkuluMawasiliano

Soma zaidi »

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwawezesha mabondia kunufaika na vipaji vyao.

Ametoa Wito huo jana (Alhamisi, Desemba 26, 2024) wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam. “Awali michezo hii ilikuwa ni ridhaa, lakini kwasasa tumeweka sheria ambazo zinataka mchezo huu uwe wa kulipwa, ambayo mchezaji …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwa njia ya Simu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipopiga simu kuzungumza na wadau na Mashabiki wa mchezo wa ngumi, wakati wa tukio maalum la pambano la ngumi la ‘Knockout ya Mama’ linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Desemba 26, 2024

Soma zaidi »

HATUA CHANYA+ ZA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) NA MATARAJIO YA KUKAMILIKA

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam umeendelea kupiga hatua muhimu katika kuboresha usafiri wa umma. Hadi sasa, Awamu ya Kwanza imekamilika na inafanya kazi, ikihusisha kilomita 21.1 kutoka Kimara hadi Kivukoni/Morocco/Gerezani, na kuhudumia wastani wa abiria 179,000 kwa siku. Awamu ya Pili, yenye urefu wa kilomita …

Soma zaidi »

HERI YA SIKUKUU YA NOELI!

Tunawatakia Watanzania wote furaha, amani, na upendo katika kipindi hiki cha Noeli. Tuwe na muda wa kusherehekea pamoja na familia na marafiki, huku tukikumbuka maana halisi ya sikukuu hii—upendo, ukarimu, na mshikamano. Mungu aendelee kuibariki nchi yetu Tanzania na kutupa mwaka mpya uliojaa matumaini na mafanikio. Noeli Njema na Mwaka …

Soma zaidi »

Ujenzi wa Kituo cha Afya Igava, Kijiji cha Igunda Muungano, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Unaendelea kwa Kasi

Kazi ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Igava kilichopo Kijiji cha Igunda Muungano, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, inaendelea kwa kasi. Ujenzi huu unafadhiliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 400, zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Fedha hizi ni …

Soma zaidi »

Ushirikiano wa Wananchi na Serikali katika Kuboresha Huduma za Afya

Kituo cha Afya Kafita, kilichopo katika Wilaya ya Nyang’hwale, Kata ya Kafita, kijiji cha Kafita, ni mfano wa mafanikio ya ushirikiano kati ya wananchi, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), na serikali kuu. Ujenzi wa kituo hiki umegharimu jumla ya shilingi milioni 200, fedha ambazo zilitokana na juhudi za wananchi, …

Soma zaidi »

Shule ya Sekondari ya Geita Girls imekuwa miongoni mwa miradi muhimu ya serikali inayolenga kuboresha sekta ya elimu nchini Tanzania. Hadi sasa, ujenzi wa shule hii umegharimu takribani TZS bilioni 4.35. Shule hii imeanza kupokea wanafunzi, na tayari zaidi ya wanafunzi 100 wapo shuleni hapo wakijifunza katika mazingira bora na ya kisasa

Licha ya mafanikio haya, juhudi za ujenzi bado zinaendelea. Mabweni ya kisasa yamepangwa kujengwa ili kuhakikisha wanafunzi wanapata sehemu salama za kuishi, na ukumbi wa mikutano unaendelea kujengwa kwa lengo la kuwapa wanafunzi na walimu nafasi ya kushiriki mikutano na shughuli mbalimbali za kitaaluma na kijamii. Kuimarisha Usawa wa Kijinsia …

Soma zaidi »

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilomita 2.3

Hafla hiyo ilifanyika katika mkoa wa Simiyu, ambapo Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ipo imara na imejidhatiti kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote nchini. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Majaliwa aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi …

Soma zaidi »