Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya nchini. DCEA inatekeleza jukumu hili kwa kutumia nguzo kuu nne ambazo ni: kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya, kupunguza uhitaji, kudhibiti madhara na kuimarisha ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.
Kupitia operesheni mbalimbali zilizofanyika kwa mwaka, Julai 2024 hadi Juni 2025, mamlaka imefanikiwa kukamata tani 2,327,983.8 za dawa za kulevya zikiwemo bangi, mirungi, skanka, heroine, metamphetamine, hashishi, cocaine na dawa tiba zenye asili ya kulevya. Hatua hizi zimepunguza kwa kiasi kikubwa mzunguko wa dawa hizo mitaani na kudhoofisha mitandao ya usafirishaji haramu.
Mamlaka pia inaendelea kutoa elimu kwa umma, hasa vijana, ili kupunguza uhitaji wa dawa hizo. Aidha, kwa kushirikiana na nchi jirani na mashirika ya kimataifa, DCEA inahakikisha mipaka inalindwa na taarifa za kijasusi zinashirikishwa kwa wakati. Mafanikio haya ni ushahidi kuwa mapambano haya yana tija, lakini yanahitaji kuungwa mkono na jamii nzima.
Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+