Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa nguzo ya kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa na kufanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali za maendeleo

Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wake, Rais Dkt. Samia ameweza kusimama imara katika kuendeleza miradi ya kimkakati na huduma za jamii, kusimamia demokrasia, kujenga uchumi na kuimarisha diplomasia.

Amesema hayo leo (Alhamisi, Juni 26, 2025) wakati alipotoa hoja ya kukamilisha shughuli za Bunge la 12, Bungeni jijini Dodoma.

“sina shaka nyote mtakubaliana nami kuwa hulka yake na ustahimilivu wake umekuwa faraja kwetu sisi wasaidizi wake, watumishi wote wa umma na Watanzania wote kwa ujumla. Isitoshe, Mheshimiwa Rais wakati wote amekuwa nguzo ya kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa.

” Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa Mwalimu wa subira, kielelezo cha ujasiri, ustahimilivu na alama ya matumaini kwa kizazi hiki. “Ni kiongozi aliyetoa mfano wa kuwa mwanamke anaweza kuongoza hata kwenye nafasi ya Kitaifa.

” Kadhalika, Majaliwa amesema kuwa kutokana na uongozi dhabiti wa Rais Dkt. Samia, taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zimetambua mchango na maono yake katika kusimamia shughuli za kimaendeleo nchini na kuitangaza Tanzania nje ya nchi.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *