Mwanza, 19 Juni 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza na wananchi katika viwanja vya Chuo cha Ufundi Kalwande, jijini Mwanza, mara baada ya kuzindua rasmi Daraja la JP Magufuli (Kigongo–Busisi) lenye urefu wa kilomita 3.0.
Katika hotuba yake, Rais Samia amepongeza juhudi za watanzania na wataalamu wa ndani kwa kukamilisha mradi huo mkubwa wa kimkakati, akisisitiza kuwa daraja hilo ni alama ya uendelezaji wa ndoto ya Hayati Dkt. John Magufuli na ishara ya kasi ya maendeleo inayoendelea chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.