Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANESCO, mafanikio haya yanatokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali kupitia miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme. Miradi hiyo inajumuisha matumizi ya vyanzo vya maji, gesi asilia, na nishati jadidifu kama vile upepo na jua.
TANESCO imeeleza kuwa maendeleo haya yanalenga kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na umeme wa kutosha kwa ajili ya matumizi ya majumbani, viwandani, na miradi ya maendeleo, sambamba na kuimarisha huduma za kijamii.
Aidha, TANESCO imeahidi kuendelea kuboresha miundombinu ya usambazaji wa umeme ili kuhakikisha huduma bora na ya uhakika inapatikana kwa wananchi wote nchini.
Hatua hii ni ishara ya juhudi za serikali za kuboresha sekta ya nishati na kuifanya kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi wa taifa. #MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya @samia_suluhu_hassan Ikulu Tanzania
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+