Taarifa hii imetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange, wakati akijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Chaya, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki. Dkt. Chaya alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kupeleka jokofu la kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya cha Nkonko.
Katika majibu yake, Mheshimiwa Dkt. Dugange alimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kuhakikisha suala la ununuzi wa jokofu hilo linapewa kipaumbele, ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma hiyo muhimu.
Aidha, katika kujibu swali la pili la Mheshimiwa Dkt. Chaya kuhusu ujenzi wa vituo vya afya vya kimkakati nchini katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25, Dkt. Dugange alieleza kuwa Serikali iko katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika majimbo yote 214 nchini.Katika majibu yake, Mheshimiwa Dkt. Dugange alimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida kuhakikisha suala la ununuzi wa jokofu hilo linapewa kipaumbele, ili wananchi wa eneo hilo wapate huduma hiyo muhimu.
Alisema, “Serikali imeshatoa taarifa na maamuzi kupitia Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba majimbo yote 214 yatapewa vituo vya afya vya kimkakati. Tayari tuko katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwa ajili ya kujenga vituo hivyo, ingawa majimbo 18 bado hayajawasilisha mapendekezo ya kata zinazohitaji kujengwa vituo hivyo vya afya.”
Hatua hizi zinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za uhakika katika maeneo yao ya karibu.
#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+