TANZANIA YAINUA BAJETI YA KILIMO HADI TRILIONI 1.3 WAKATI DUNIA IKIKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MAVUNO!

Sekta ya kilimo nchini Tanzania inaendelea kupewa kipaumbele na serikali kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza ajira. Bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka shilingi bilioni 294 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi shilingi trilioni 1.3 mwaka wa fedha 2024/2025, ikionyesha dhamira ya serikali katika kuimarisha sekta hii muhimu.

Kwa sasa, sekta ya kilimo inachangia takriban asilimia 26 ya Pato la Taifa, sawa na shilingi trilioni 38. Aidha, inatoa ajira kwa takriban watu milioni 18.6 nchini.

Katika ngazi ya kimataifa, Baraza la Kimataifa la Nafaka (IGC) limepunguza makadirio ya uzalishaji wa ngano duniani kwa msimu wa 2024/2025 kwa tani milioni 2, kufikia tani milioni 796. Hii inatokana na mavuno duni katika Umoja wa Ulaya, hususan Ufaransa na Ujerumani, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Hata hivyo, uzalishaji wa mahindi duniani unatarajiwa kuongezeka kwa tani milioni 1, kufikia tani bilioni 1.225, huku Afrika ikitarajiwa kuzalisha tani milioni 91. Uzalishaji wa soya pia umepunguzwa kwa tani milioni 2, kufikia tani milioni 419, kutokana na makadirio ya chini ya mavuno nchini Marekani.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *