Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameungana na maelfu ya wananchi katika kusherehekea Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya Ziwa, lililofanyika leo tarehe 21 Juni, 2025. Tamasha hili limekuwa jukwaa muhimu la kuenzi urithi wa kitamaduni, sanaa, ngoma, mavazi ya asili na mila za watu wa Kanda ya Ziwa.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kulinda, kuenzi na kuendeleza tamaduni za Kitanzania kama msingi wa umoja, amani na maendeleo. Aidha, amewapongeza waandaaji wa tamasha kwa kukuza utalii wa ndani na kutoa fursa za kiuchumi kwa wasanii na wajasiriamali wa maeneo ya kanda hiyo.
#BulaboFestival2025 #RaisSamia #UtamaduniKwanza #KandaYaZiwa #Tanzania