Maktaba ya Mwezi: September 2025
NEMC kanda ya Kusini katika kuadhimisha siku ya Usafi duniani wamesafisha fukwe za Call and Vision Manispaa ya Mtwara Mikindani
NEMC Kanda ya Ziwa Mashariki katika kuadhimisha siku ya usafi duniani wamefanya usafi Soko la Samaki nyamagana
NEMC YAANZA UKAGUZI WA MAZINGIRA KWA MIRADI YA MAENDELEO
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetunukiwa Tuzo Kuu ya Ubunifu katika Huduma Jumuishi za Fedha (Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award) inayotolewa na Jumuiya ya Huduma Jumuishi za Fedha (AFI), yenye wanachama 84 duniani.
Tuzo hiyo ilipokelewa na Naibu Gavana wa BoT anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, kwa niaba ya Gavana Bw. Emmanuel Tutuba, katika Mkutano Mkuu wa AFI uliofanyika hivi karibuni mjini Swakopmund, Namibia. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 15, 2025 wakati akitangaza tuzo hiyo, …
Soma zaidi »Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetunukiwa Tuzo Kuu ya Ubunifu katika Huduma Jumuishi za Fedha (Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award) inayotolewa na Jumuiya ya Huduma Jumuishi za Fedha (AFI), yenye wanachama 84 duniani.
Tuzo hiyo ilipokelewa na Naibu Gavana wa BoT anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Bi. Sauda Msemo, kwa niaba ya Gavana Bw. Emmanuel Tutuba, katika Mkutano Mkuu wa AFI uliofanyika hivi karibuni mjini Swakopmund, Namibia. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Septemba 15, 2025 wakati akitangaza tuzo hiyo, …
Soma zaidi »HABARI KWA UMMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Japan Mhe. Anderson Mutatembwa, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma
Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amemsihi Balozi Mutatembwa kuzingatia kipaumbele cha nchi ambacho ni diplomasia ya uchumi kwa kuhakikisha anavutia wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchini Japan pamoja na kuimarisha ushirikiano wa ubia. Amemsisitiza Balozi Mutatembwa kuhakikisha makampuni ya Japan yanawekeza nchini Tanzania ili kuongeza thamani ya bidhaa hapa nchini …
Soma zaidi »Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu Kailima, R. K (kulia) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndugu Adam Mkina wakishuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – WAZALENDO), Mhe. Luhaga Joelson Mpina na Mgombea Mwenza, Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej majira ya Saa 10:00 jioni ya leo (13/9/2025)
Ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria inayotaka fomu hizo kubandikwa kwa Saa 24 ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa …
Soma zaidi »WATUHUMIWA 940 MBARONI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imekamata kilogramu 33,077.623 za dawa za kulevya aina mbalimbali huku ikiwashikilia watuhumiwa 940 kuhusika kwenye matukio tofauti ya uhalifu wa dawa za kulevya. Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, akizungumuza na waandishi wa Habari leo Septemba 8,2025 jijini Dar …
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+