Maktaba ya Kila Siku: September 8, 2025

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka taasisi na asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na weledi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 08 Septemba, 2025 wakati akifungua kikao kazi cha Tume na taasisi na asasi hizo kilichofanyika Mkoani Dodoma. “Ni vyema mkafahamu kuwa kifungu cha 10(1)(g) na (h) cha Sheria ya Tume Huru …

Soma zaidi »

Wanasayansi wanawake wawili – Profesa Mary Abukutsa-Onyango kutoka Kenya na Mercy Diebiru-Ojo kutoka Nigeria – wametangazwa washindi wa Tuzo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2025 (Africa Food Prize 2025).

Tuzo hiyo, yenye thamani ya Dola za Marekani 100,000, ilikabidhiwa na Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Chakula Barani Afrika. Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika mjini Dakar, Senegal, pembezoni mwa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AFSF) linaloendelea …

Soma zaidi »