Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais.

Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar.

Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

#KurayakoHakiyakoJitokezeKupigaKura #oktoba2025 #tumehuruyataifayauchaguzi #uchaguzi2025 #UchaguziMkuu #uchaguzi

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA AZUNGUMZA MARA BAADA YA KUAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa hotuba muhimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *